NEEC wafanya kikao na Mfuko wa kuchochea Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Catalytic Trust)

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limekutana na Mfuko wa kuchochea Kilimo Tanzania (TACT) katika Makao Makuu yake Dodoma huku lengo kuu ni kuuelewa Mfuko huo na shughuli zake pamoja na kuona namna watakavyoshirikiana.

Ugeni huo uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko Dr. John Kyaruzi akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Biashara Dr. Juma Makaranga.

Katika kikao hicho Dr. Kyaruzi alifanya wasilisho kuhusu Mfuko kwa Menejimenti ya Baraza ikiongozwa na Katibu Mtendaji Bibi. Beng’i Issa na baadaye kujadiliana mambo kadhaa katika kuwawezesha wakulima wa Tanzania.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bibi. Beng’i Issa ambaye alikuwa Mwenyekiti.