NAIBU Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akielezea jambo alipotembele makao makuu ya Mfuko wa SAGCOT Kichocheo yaliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza toka ateuliwe na Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.
NAIBU Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizungumza jambo na watendaji wa Mfuko wa SAGCOT Kichocheo(SAGCOT Catalytic Trust Fund [CTF]) alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza toka ateuliwe na Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.
SAGCOT Kichocheo (SAGCOT Catalytic Trust Fund [CTF]) imepongezwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Bw. Innocent Bashungwa,kwa kuwainua wakulima wadogo na kuwaingiza katika kilimo chenye tija.
Ameiambia hafla katika ofisi za mfuko huo baada ya kutembelea taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam kwamba kilimo chenye tija kitachagiza maendeleo ya haraka kwa Taifa.
Bw. Bashungwa amesema Serikali imejipanga kuhahikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati, kuwapa mitaji na kutafuta masoko kwa mazao yote ya kimkakati ili kufikia adhima ya serikali ya kutokomeza umasikini unaowakabili wakulima na Taifa kwa ujumla
“Serikali inafanya jitihada kubwa katika kumtafutia mkulima masoko ya mazao yake, kuagiza pembejeo nje ya nchi ili mkulima azipate kwa bei nafuu pamoja na kuwapa mitaji kupitia taasisi zake mbalimbali ,” amesema Bw. Bashungwa, na kuongeza kwamba Serikali imejipanga kuhahikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati, mitaji na masoko.
Ametoa ameushauri mfuko kushirikiana na taasis nyingine zinazojihusisha moja kwa moja na kilimoi kubuni mpango endelevu wa kumsaidia mkulima kushinda umaskini. Ametaja taasisi za aina hiyo kuwa ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
“Nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnazozifanya licha ya changamoto kadhaa mlizonieleza. Kwa ushirikiano wenu na wadau wa sekta hii na mipango iliyopo tutafikia malengo ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kwa kujenga viwanda. Tukumbuke kuwa kilimo kinaajiri zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania na ni chanzo kikubwa cha malighafi,” amesema Naibu Waziri huyo.
Katibu Mtendaji wa mfuko huwo, Bw. John Kyaruzi, amemshukuru Naibu Waziri kwa ziara yake na kueleza kwamba imetoa fursa kwa mfuko kueleza mafanikio na changamoto ambazo wanakutananazo katika kutimiza malengo yake.
“Hii ni fursa adhimu kutembelewa na Naibu Waziri, tunashukuru sana na tumetumia nafasi hii kueleza mambo tunayokabiliana nayo katika utekelezaji wa majukumu yetu.” Alisema Bw. Kyaruzi
Bw. Kyaruzi alimhakikishia Waziri kuwa taasisi yake itayafanyia kazi mapendekezo yote kwani kimsingi yatamsaidia mkulima kutokana na umasikini kwa kuenzi kilimo chenye tija.
Tangu kuanzishwa kwa mfuko umejenga maghala katika maeneo mbalimbali katika mikoa ya nyanda za juu kusini, umetoa wa mikopo yenye masharti nafuu, kusambaza pembejeo na kwa wakulima wadogo.
SOURCE: THE Citizen